Home News Picha: Mfahamu zaidi, Jane ‘Pacha’ wa Rich Mavoko kwenye video yake mpya

Picha: Mfahamu zaidi, Jane ‘Pacha’ wa Rich Mavoko kwenye video yake mpya

Picha: Mfahamu zaidi

Afrika Kusini kama kama nchi zingine zilizoendelea zinaichukulia kazi umodel kwa uzito mkubwa na ndio maana ilimcost Rich Maviko mkwanja mrefu kidogo kupata huduma za binti mrembo anayeonekana kwenye video ya ‘Pacha Wangu’.

Binti huyo anaitwa Jane, mzaliwa wa Afrika Kusini na ni kutoka kampuni ya D&A iliyopo jijini Cape Town. Jane ameshafanya kazi kubwa mbalimbali za modeling kama fashion shows pamoja na kutokea kwenye majarida ya urembo mbalimbali ikiwemo lile kubwa la Maybelline la nchini Marekani.

“Haikuwa rahisi kumpata sababu kule tumeenda hatujuani na watu kivile, ila wenzetu kila kitu chao kipo kwenye internet, so tulichofanya tukawatafuta mwisho na tukapewa machaguo kibao, na huwezi amini msichana tuliyetakiwa kushoot naye hakuwa huyu,” Mavoko ameiambia JOHVENTURE MUSIC.

“Jane tumempata mwishoni kabisa dakika ya 90, aliyetakiwa kushoot na sisi alikuwa anaitwa Bibi, sema akapata safari ya ghafla nje ya Afrika Kusini yenye mtonyo zaidi ndo tukaja kumvumbua Jane ambaye kawa mkali kuliko yule.”

Huyu ndiye Bibi, msichana aliyekuwa amepangwa kuonekana kwenye video hiyo

Tazama picha zaidi za Jane hapo chini.

 

 

Previous articleDiamond atajwa kuwania tuzo nyingine kubwa Nigeria,’THE HEADIES 2014’
Next articleNew VIDEO | Dj Jimmy Jatt ft Banky W & Phyno – E To Beh | Download