Navy Kenzo Katika album ya wasanii wa label ya Empire Africa, Kupitia mtandao wa Billboard, Hot97 na gazeti la Variety la nchini marekani, kundi la muziki kutoka Tanzania Navy Kenzo linalo undwa na wasanii Aika na Nahreel, wametajwa kuwa ni moja wapo ya wasanii watakao unda track list ya album iliyoandaliwa na kampuni ya usambazaji wa muziki ya EMPIRE iliyopo San Francisco Marekani, Album ambayo itakuwa na mjumuisho wa mastar wa muziki kutoka Africa wakiwemo
Olamide, Fireboy DML, Kizz Daniel, Buju BNXN, Asake, Black Sherif na wengineo wengi.Album hiyo imepewa jina la “Where we come from (Tulipo toka)” wamefanya hivyo baada ya muziki kutoka barani Africa
kusikilizwa na kupendwa kwa kiwango kikubwa duniani na kwa mujibu wa tovuti hizo Album hiyo inatarajiwa kutoka mwezi
November tarehe 18