Home News It’s a baby girl: Zari na Diamond wapata mtoto wa kike

It’s a baby girl: Zari na Diamond wapata mtoto wa kike

Zari na Diamond wapata mtoto wa kike

It’s a baby girl: Zari na Diamond wapata mtoto wa kike

Diamond Platnumz na Zari the Bosslady wamepata mtoto wa kike.

Mtoto huyo ameingia duniani Alhamis hii. Haijaweza kufahamika kwa mara moja ni hospitali gani mtoto huyo amezaliwa kwa kile meneja alichosema ‘usalama wa mama na mtoto’ kwakuwa bado wapo hospitali.

Awali Diamond alisema kuwa Zari angejifungulia Tanzania . Jina la mtoto huyo halijaweza kufahamika kwa sasa.

 

Jina watakuja nalo baadaye maana bado hawajaamua,” meneja wa Diamond, Salam Sharaff ameiambia JohVentureBlog.

 

Hivi karibuni wakati akizungumza na Mambo Mseto na Willy M. Tuva wa Radio Citizen ya Kenya, Diamond alisema anataka mtoto wake azaliwe nyumbani Tanzania.

Diamond na Zari wote walikuwa na jina ambalo wangependa kumuita mtoto wao ambapo Zari alitaka wamuite mtoto wao Zara huku Diamond naye akitaka amuite Candy.

 

Hata hivyo Diamond alisema wamekubaliana watafute jina litakalokuwa katikati lakini lenye maadili ya dini ya Kiislam.

 

Tunawapongeza mastaa hao.

You may also like; WATCH| Diamond Platnumz Essence Festival Of Culture Virtual Experience

Previous articleDownload | M-Rap Ft MisRiz – Hawajui [New Video]
Next articleDownload | Galaxy – Mzuri tu [New Audio]