Home News Dayna Nyange:Juhudi bila ya Wadau ngumu kutoboa nje

Dayna Nyange:Juhudi bila ya Wadau ngumu kutoboa nje

Dayna Nyange:Juhudi bila ya Wadau ngumu kutoboa nje

Dayna Nyange:Juhudi bila ya Wadau ngumu kutoboa nje 

Mwanamuziki Dayna Nyange ametoa mtazamo wake wa namna gani wasanii wa nyumbani watawezakuvuka mipaka ya nje ya nchi

Alipokuwa anafanyiwa mahojiano na mwandishi wa habari hii Dayna
alifunguka kwamba ili wasanii waweze kutoboa ni lazima wawe na Wadau wa
nje (connection) kwani wengi wanafanya kazi nzuri lakini kutokuwa na
wadau ndio kikwazo.

“Msanii kama Vanessa Mdee leo hii anaanza kuvuka boda ni kwa sababu
ya connection ya watu wa nje alionao, kama aliweza kufanya kazi na watu
wa MTV sasa kwa nini asifike mbali ukizingatia anafanya kitu kizuri”,
alifafanua Dayna.

Dayna alieleza pia kuhusu ujio wa video ya wimbo wake wa Nitulize
aliomshirikisha Nay wa Mitego kwamba wataanza kuirekodi siku chache
zijazo kwani kuna vitu muhimu wanasubiri kutoka nje ya nchi.

Video hiyo inatarajiwa kurekodiwa hapahapa nyumbani Tanzania, huku
akisita kuweka wazi ni kampuni gani ambayo itatengeneza video hiyo na
kusema watu wasubiri Surprise.

Dayna mwanamuziki huyu mwenye asili ya mkoani Morogoro mwisho
alitoa taarifa kwa mashabiki wake wa Tanga wakae sawa kwani anatarajia
kuanza show zake mkoani humo kuanzia sikukuu ya Eid.

You may also like; Dayna Nyange Ft. Bill Nass – KOMELA | Mp3 Download [New Song]

Previous articleOfficial Video HD | Nay Wa Mitego – Sina Muda | Watch & Download
Next articleOfficial Video HD | Real Jofu Ft. Ney Lee – Kumbe Ni Ndugu | Watch & Download