Home Uncategorized VIDEO:WCB wamkamata anayetukana Instagram kwa kutumia jina la Shilole

VIDEO:WCB wamkamata anayetukana Instagram kwa kutumia jina la Shilole

0

Mitandao ya kijamii imetoa uwanja mpana
wa kila aliyejiunga kutoa maoni yake au kuandika chochote kwenye page
yake au page za wenzake ambapo uhuru huu umepelekea tuone wengine
wakitukanwa au kuandikwa vibaya.
Asubuhi ya November 18 2016 Meneja wa Diamond Platnumz na Tiptop Connection Babu Tale amethibitisha kukamatwa kwa kijana wa Kitanzania ambaye anatuhumiwa kutoa matusi kupitia Instagram.
Tale ameandika ‘Kama
unajua ulishawahi kumtuma huyu dogo atukane watu ujue sheria ipo
mlangoni kwako na huyu atakua mfano, hapa alikua anawataja waliomtuma……
serikali ikiamua hata ujifiche wapi utakamatwa tu so endeleeni kutukana
watu msiowajua, anajiita Shilole Kiuno’
Mwanachama mwingine wa WCB aliyetoa maoni yake kuhusu hii ni dancer wa Diamond Mose Iyobo >>> ‘Huyu ndio mwenye account ya @Shilolekiuno_official mavuno ya matusi yake ni pingu alikua anajiona mjanja mwenyewe leo kayakanyaga
‘Muone anavyotia huruma sema amekamatwa
wakati huruma amesafiri ndio kichwa kinapomuuma na mpaka aje kurudi
huyu Huruma Dar imeshakua ya Madereva sio Makonda tena‘ – Mose Iyobo

VIDEO: Ni comment gani mbaya imewahi kumuumiza Diamond Platnumz? bonyeza play kwenye hii video hapa chini

Facebook Comments