Home Uncategorized Dj Fetty wa Clouds Fm atangaza kuacha kazi ya utangazaji, aagwa rasmi...

Dj Fetty wa Clouds Fm atangaza kuacha kazi ya utangazaji, aagwa rasmi Sept 15 kwenye XXL

0

Aliyekuwa mmoja wa watangazaji wa kipindi maarufu cha burudani XXL cha Clouds FM, Fatma Hassan ‘Dj Fetty’ leo Sept.15,2015 amewaaga rasmi wasikilizaji na wafanyakazi wenzake na kuachana na kazi ya utangazaji ili kuendeleza kibiashara zake.

Fetty amesikika kwenye kipindi hicho leo kwa mara ya mwisho kama sehemu ya kusema kwaheri.

Fetty akiagwa na wafanyakazi wenzake kwenye XXL

Kipindi hicho ambacho huongozwa na B Dozen akishirikiana na Adam Mchomvu sasa kimepata member mpya, Kennedy The Remedy aliyechukua nafasi ya Fetty.

Kennedy The Remmedy (kushoto) aliyeungana na familia ya XXL

Facebook Comments