Home Uncategorized Belle 9 adai video za muziki za Kibongo zinafanana, apanga kuja na...

Belle 9 adai video za muziki za Kibongo zinafanana, apanga kuja na kitu tofauti

0

Belle 9 amedai anajiandaa kufanya video ya wimbo wake ‘Shauri Zao’ kwa utofauti mkubwa kwakuwa amebaini video nyingi za Bongo Flava zinafanana.

Akiongea na E-Newz ya EATV, Belle alisema:

Unajua sasa hivi video nyingi ukiangalia zinafanana location. Siwezi kuzitaja hizo video, sikupenda sasa hivi video itoke kwa kuwa sitaki ifanane na zingine ndio maana tunatumia muda mrefu kutafuta location ili iwe tofauti na video zingine na iwe video ambayo inaendana na wimbo. Kazi zangu mashabiki wanazijua na kila ngoma inayotoka huwa kali zaidi ya ile na sidhani kama kuna msanii anaweza kuwa hivyo kama mimi.” 

Facebook Comments